HISTORIA YETU

UTANGULIZI


TANROADS SACCOS LIMITED ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), waliokuwa watumishi wa Wakala ya Barabara (TANROADS) na Watumishi waajiriwa wa TANROADS SACCOS LIMITED.

USAJILI


Chama kiliandikishwa kwa mara ya kwanza Julai 27, 2006 na kupewa namba ya Usajili DSR 896. Mwaka 2021 Chama kilisajiliwa kwa mujibu wa Sheria Na. 10 ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019 na kupewa Leseni ya Mtoa Huduma Ndogo za Fedha namba MSP3-TCDC/2021/0418. 

Hata hivyo mnamo Mei 03, 2023 Chama kilisajiliwa upya na TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA TANZANIA (TCDC) na kupewa namba mpya ya usajili PRI-DAR-DAR-CC-2023-5373

Maono

Kubadilisha maisha ya wanachama kwa kuwapa huduma za kifedha zilizo bora, rahisi na za haraka.

Dira

Kuwa taasisi bora ya fedha na rafiki kwa wanachama kwa uchumi wa mwanachama inayotoa huduma za kifedha kwa masharti nafuu.

Malengo

Kuwa chombo cha kiuchumi kilichoanzishwa na kusimamiwa na wanachama wenyewe.

THAMANI YETU


MALENGO YA KIMKAKATI


Mafanikio Yetu Kitaifa

TANROADS SACCOS LIMITED imetambuliwa rasmi na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kuwa miongoni mwa Vyama Bora 20 vya Ushirika nchini, ikiongoza katika viashiria vikuu vya ufanisi wa kiuchumi.

🏆

Ziada Kubwa Kabla ya Kodi ya Mapato

Mwaka 2024
Nafasi ya 8 (📈 Kupanda)
Mwaka 2023
Nafasi ya 14
💰

Bakaa ya Akiba na Amana za Wanachama

Mwaka 2024
Nafasi ya 18
Mwaka 2023
Nafasi ya 17
📊

Bakaa ya Mikopo kwa Wanachama

Mwaka 2023
Nafasi ya 20

Inadhihirisha uaminifu na ukwasi mkubwa katika kuhudumia mahitaji ya mikopo.

🏢

Kiwango Kikubwa cha Rasilimali (Assets)

Mwaka 2023
Nafasi ya 20

Inathibitisha uimara wa mtaji na ukuaji endelevu wa rasilimali za chama.

TANROADS SACCOS LIMITED ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS).

Jengo la Wizara, ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Gorofa ya Tatu, Chumba Namba 5, Kitalu Na. 10 Makutano ya Mtaa wa Shaaban Robert na Garden

+255-738 749 253 / +255-796 250 187

saccos@tanroads.go.tz

Huduma zetu

Bidhaa zetu

Scroll to Top