tanroadsacoos_bg
previous arrow
next arrow

UJUMBE WA MWENYEKITI


Kwa niaba ya Bodi, Menejimenti na Wanachama wa TANROADS SACCOS LIMITED, ninayo furaha kubwa kukukaribisha kutembelea tovuti yetu rasmi. Tovuti hii imeandaliwa kwa lengo la kuwapatia wanachama, wadau na umma kwa ujumla taarifa sahihi kuhusu shughuli, huduma, bidhaa na maendeleo mbalimbali ya Chama chetu. Tunaamini kuwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni nyenzo muhimu katika kuimarisha uwazi, uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa Wanachama wetu. 

TANROADS SACCOS LIMITED ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo kilichosajiliwa kwa mujibu wa Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuwawezesha Wanachama wake kiuchumi kupitia huduma za kuweka Akiba, kununua Hisa na kutoa mikopo kwa Wanachama wake. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006, Chama kimeendelea kukua na kuimarika kutokana na ushiriki wa wanachama wake, uongozi thabiti na usimamizi bora wa rasilimali.Kupitia tovuti hii utaweza...

UJUMBE WA MWENYEKITI

Kwa niaba ya Bodi, Menejimenti na Wanachama wa TANROADS SACCOS LIMITED, ninayo furaha kubwa kukukaribisha kutembelea tovuti yetu rasmi. Tovuti hii imeandaliwa kwa lengo la kuwapatia wanachama, wadau na umma kwa ujumla taarifa sahihi kuhusu shughuli, huduma, bidhaa na maendeleo mbalimbali ya Chama chetu. Tunaamini kuwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni nyenzo muhimu katika kuimarisha uwazi, uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa Wanachama wetu.

TANROADS SACCOS LIMITED ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo kilichosajiliwa kwa mujibu wa Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuwawezesha Wanachama wake kiuchumi kupitia huduma za kuweka Akiba, kununua Hisa na kutoa mikopo kwa Wanachama wake. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006, Chama kimeendelea kukua na kuimarika kutokana na ushiriki wa wanachama wake, uongozi thabiti na usimamizi bora wa rasilimali.

Kupitia tovuti hii utaweza kupata taarifa mbalimbali ikiwemo bidhaa za mikopo na akiba, taarifa za utendaji wa Chama, matangazo muhimu, fursa mbalimbali, pamoja na habari zinazohusu maendeleo ya Chama. Aidha, tunatarajia tovuti hii kuwa daraja muhimu la mawasiliano kati ya Chama na wadau wake wote.

Bodi ya Chama itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mipango na mikakati inayolenga kuongeza thamani kwa Wanachama, kuimarisha uthabiti wa kifedha wa Chama na kukuza ustawi wa kijamii na kiuchumi wa Wanachama wetu.

Tunawashukuru Wanachama wetu kwa imani na ushirikiano wanaoendelea kuuonyesha kwa Chama. Vilevile, tunawashukuru wadau wote wanaoshirikiana nasi katika safari ya kujenga taasisi imara, endelevu na yenye mchango chanya kwa maendeleo ya sekta ya ushirika nchini.

Karibu sana TANROADS SACCOS LIMITED.

Bw. Meritus M. Njeama

Mwenyekiti wa Bodi

Maono

Kubadilisha maisha ya wanachama kwa kuwapa huduma za kifedha zilizo bora, rahisi na za haraka.

Dira

Kuwa taasisi bora ya fedha na rafiki kwa wanachama kwa uchumi wa mwanachama inayotoa huduma za kifedha kwa masharti nafuu.

HUDUMA NA BIDHAA ZETU


TANROADS SACCOS LIMITED tunatoa huduma za kifedha na bidhaa mbalimbali kwa wanachama wetu, zenye lengo la kukuza akiba, kutoa mikopo nafuu, na kuboresha ustawi wao wa kifedha.

Huduma hii inawawezesha wanachama kununua hisa ili kuongeza umiliki wao na kuimarisha mtaji wa chama.

Huduma hii inawawezesha wanachama kuweka akiba kwa usalama ili kufikia malengo yao ya kifedha.

Huduma hii inawawezesha wanachama kupata mikopo kwa masharti nafuu ili kukidhi mahitaji yao ya kifedha.

Huduma hii inahakikisha wanachama wanarejesha mikopo yao kwa utaratibu uliowekwa ili kuendeleza ufanisi wa chama.

Kwa ajili ya miradi ya maendeleo na uwekezaji wa muda mrefu.

Kwa kukidhi mahitaji ya haraka ya kifedha ya muda mfupi.

Kwa ajili ya dharura zisizotarajiwa.

Kusaidia kugharamia elimu na mahitaji ya masomo.

Kwa maandalizi ya sikukuu na shughuli za kijamii.

Kwa maandalizi ya sikukuu na shughuli za kijamii.

Mahususi kwa watumishi wa TANROADS SACCOS LIMITED.Provide your feedback on BizChat

KWANINI UTUCHAGUE


Kujiunga na TANROADS SACCOS LIMITED ni hatua muhimu ya kujenga ustawi wa kifedha na kufikia malengo yako ya kiuchumi. Chama kinatoa fursa mbalimbali zinazowawezesha Wanachama kunufaika na huduma bora za kifedha katika mazingira salama na ya kuaminika.
Faida za Kujiunga na TANROADS SACCOS LIMITED

TAKWIMU


WANACHAMA

Kuishia Disemba, 24 2024

1,919

Jumla ya wanachama

MALI

Kuishia Disemba, 24 2024

TZS 9.67B

Jumla ya mali

MIKOPO

Kuishia Disemba, 24 2024

TZS 7.17B

Jumla ya mikopo

MIAKA

Tangu mwaka 2007

20+

Miaka ya huduma

MATUKIO


Siku ya Wanachama

Siku ya Wanachama ni moja ya matukio muhimu na yenye thamani kubwa ndani ya TANROADS SACCOS LIMITED. Tukio hili huandaliwa kwa lengo la kuwakutanisha wanachama wote katika mazingira ya urafiki...

TANROADS SACCOS LIMITED ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS).

Jengo la Wizara, ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Gorofa ya Tatu, Chumba Namba 5, Kitalu Na. 10 Makutano ya Mtaa wa Shaaban Robert na Garden

+255-738 749 253 / +255-796 250 187

saccos@tanroads.go.tz

Huduma zetu

Bidhaa zetu

Scroll to Top