UANACHAMA
Home » Uwanachama
KUKIDHI UANACHAMA
Mtumishi wa TANROADS aliye katika ajira ya kudumu, ajira ya mkataba, mstaafu au mtumishi aliyeajiriwa na Chama anapata sifa ya awali ya kujiunga kwa kuzingatia msingi namba moja (1) wa Ushirika ambao ni Uanachama wa hiari na ulio wazi. Endapo atakidhi mahitaji ya Fungamano la pamoja la uanachama ni sharti awe na sifa zifuatazo :
- Awe mwenye umri wa miaka isiyopungua 18.
- Awe mwenye tabia nzuri, mwaminifu na mwenye akili timamu.
- Awe amelipa kiingilio, hisa za uanachama na kuweka akiba kwa kiwango kilichowekwa kwa mujibu wa masharti haya na awe tayari kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za Chama.
- Awe anaelewa na kuwa tayari kutekeleza madhumuni ya chama kama yalivyoainishwa kwenye masharti haya na kufafanuliwa katika nyaraka mbalimbali.
- Awe tayari kufuata Masharti ya chama, Kanuni na Sheria za vyama vya Ushirika wakati wote.
- Asiwe na shughuli yeyote ile inayofanana na kuweka au kukopesha wanachama ili kuondoa mgongano wa masilahi.
MAHITAJI YA UANACHAMA
Mwanachama tarajiwa atapaswa:
- Kujaza fomu ya kujiunga ambayo inapatikana katika ofisi ya Uongozi wa tawi alipo lakini pia fomu inapatikana katika tuvoti hii ya Chama eneo la jihudumie.
- Kulipia Ada ya Uanachama kulingana na kiasi kinachotumika kwa wakati huo. Kwa sasa Ada ya Uanachama ni Tshs 50,000/= ambazo hazirejeshi pindi mwanachama anavyojitoa.
- Kununua Hisa anzia 80 @ Tshs 10,000 zenye thamani ya Tshs 800,000.00
MCHAKATO WA USAJILI WA WANACHAMA
Maombi ya kujiunga katika Chama yatafuata utaratibu ufuatao :
- Mtumishi yoyote wa Wakala ya Barabara Tanzania atakayekuwa ametimiza masharti ya kujiunga ataomba uanachama kwa kujaza fomu ya ombi la Uanachama namba TNRDS/SACCOS/1/Uanachama iliyoandaliwa na Chama.
- Mwombaji atajadiliwa na uongozi wa Chama ili kujiridhisha iwapo anakidhi vigezo vya kuwa mwanachama na uongozi wa Chama unaweza kumkubali au kumkataa.
- Mapendekezo ya wanachama wapya yatapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu kwa uthibitisho ambapo waombaji wote waliokubaliwa na Bodi watakuwa na haki ya kuhudhuria Mkutano Mkuu huo na kujadiliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu na uamuzi wa Mkutano Mkuu utakuwa wa mwisho.
- Mwanachama akishapitishwa na Mkutano Mkuu atakuwa na haki ya kupatiwa kitambulisho cha uanachama na endapo kitambulisho kitapotea, mwanachama atapewa kitambulisho kingine kwa kulipa gharama kwa kuzingatia kiwango kitachachowekwa na bodi na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu.
ADA ZA UANACHAMA & MTAJI WA KUGAWANA
(1) Mwanachama atakapokubali kujiunga na Chama atapaswa.
- a) Kulipa kiingilio kitakachokuwa kimepangwa na Chama kwa wakati huo
- b) Kununua idadi ya Hisa zitakazokuwa zimepangwa na Chama na kuainishwa katika Sera ya Hisa kwa wakati huo hata hivyo mwanachama ataruhusiwa kulipa hisa za awali zitakazokuwa zimepangwa na kukamilisha kima cha chini ndani ya miezi 12 tangu afanye malipo ya awali
- c) Kuweka Akiba na kununua hisa kila mwezi kwa kiasi kitakachokuwa kimepangwa na Chama kwa mujibu wa Sera ya Uhamasishaji wa Akiba wakati huo.
(2) Mwanachama ambaye atashindwa kutimiza matakwa ya sharti dogo (1) (b) hapo juu hataruhusiwa kunufaika na haki za mwanachama katika Chama.
(3) Viwango vya kiingilio, hisa na akiba vinaweza kubadilishwa kwa maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Wawakilishi.
(4) Mwanachama aliyekamilisha kulipia Hisa zote atapewa hati ya kumiliki Hisa.
HAKI ZA MWANACHAMA
Mwanachama atakuwa na haki zifuatazo:
- Kushiriki kikamilifu katika shughuli za Chama ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mikutano yote anayohusika.
- Kupiga kura chini ya msingi ya mtu mmoja kura moja bila kujali idadi ya Hisa anazomiliki.
- Kuchagua na kuchaguliwa katika Uongozi wa Chama.
- Kuwa na haki sawa kuhusu mali ya Chama na kudhibiti ipasavyo matumizi yake.
- Kupatiwa huduma zozote zinazotolewa na chama ilimradi amekidhi masharti yanayoambatana na huduma hiyo.
- Kupatiwa taarifa mbalimbali za shughuli za Chama, muhtasari wa mkutano na nyaraka nyingine za chama kwa ajili ya mapitio akiwa katika ofisi za chama.
- Kuteua Mrithi.
- Kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya Bodi ya Uongozi na Mkutano Mkuu.
- Kupokea gawio na faida nyingine kutoka katika shughuli za Chama kwa kuzingatia masharti ya Chama.
WAJIBU WA MWANACHAMA
Wajibu wa mwanachama utakuwa ni pamoja na:
- Kukamilisha kununua hisa na kuweka akiba kwa kuzingatia Masharti ya Chama.
- Kufuata na kutekeleza Sheria ya Vyama vya Ushirika na Kanuni zake, Masharti ya Chama, maamuzi ya Mkutano Mkuu na maelekezo mengine halali kwa mujibu wa Sheria za nchi.
- Kurejesha mkopo kwa wakati uliopangwa.
- Kutoa michango mbalimbali katika kuendeleza madhumuni ya Chama kadri itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu.
- Kubeba dhamana endapo janga lolote litakipata Chama.
- Kuwa mwaminifu na kuonesha ushirikiano katika kutekeleza shughuli za Chama.
- Kumdhamini mkopo mwanachama mwenzake isipokuwa kama mwanachama aliyedhamini hatakuwa na haki ya kudhaminiwa na mwanachama aliyemdhamini katika kipindi kile kile.
- Kulipa mkopo alioudhamini endapo mdhaminiwa atashindwa kulipa mkopo wake.
- Kuhudhuria semina na mafunzo yanayotolewa na Chama.
TANROADS SACCOS LIMITED ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS).
Jengo la Wizara, ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Gorofa ya Tatu, Chumba Namba 5, Kitalu Na. 10 Makutano ya Mtaa wa Shaaban Robert na Garden
+255-738 749 253 / +255-796 250 187
saccos@tanroads.go.tz
Linki za haraka
Huduma zetu
- Huduma ya kununua hisa
- Huduma ya kuweka akiba
- Huduma ya mikopo
- Huduma ya kurudisha mikopo
Bidhaa zetu
- Mkopo wa maendeleo
- Mkopo wa kupumulia
- Mkopo wa Dharura
- Mkopo wa somesha
- Mkopo wa sikukuu
- Mkopo wa watumishi wa chama
